Taarifa ya Polisi kuhusu mwili wa Padri uliokutwa ndani ya tenki la maji

0
42

Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema linaendelea kuchunguza kwa kina kifo cha Paroko wa Parokia ya Mbezi Mshikamano, Padri Francis Kangwa (49), wilayani Ubungo, Dar es salaam.

Padri hiyo raia Zambia alikutwa amefariki ndani ya tenki kubwa la maji lililoko nyuma ya nyumba ya makazi ya Mapadri Mtaa wa Sokoine katika jengo la Ottoman, Dar es Salaam.

“Padri huyo alifika katika Kanisa la ‘St. Joseph’ lililopo Mtaa wa Sokoine April 12, 2022 kwa ajili ya ibada maalum, na mara baada ya ibada alielekea kwenye makazi ya Mapadri kujipumzisha lakini hakuonekana mpaka Aprili 15, 2022 alipokutwa amefariki eneo hilo,” jeshi la polisi limeeleza.

Taarifa huyo imeongeza zaidi kuwa uchunguzi wa awali kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kiuchunguzi unaonesha dalili kwamba Padri huyo anaweza kuwa amejiua.

Hata hivyo jeshi hilo limesema linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi iliyopelekea kifo cha Padri huyo.

Send this to a friend