Taarifa ya Serikali kuhusu kuanza ujenzi wa Daraja la Jangwani

0
45

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya imesema upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika kwa ajili ya ujenzi wa daraja jipya la Jangwani jijini Dar es Salaam.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Asha Juma bungeni Dodoma, Kasekenya amesema kwa sasa upo mpango wa dharura unaotumika kuhakikisha daraja la Jangwani lililopo linaendelea kutumika hata wakati wa msimu wa mvua.

“Hata hivyo yupo mkandarasi maalum ambaye kila baada ya mvua kunyesha anaondoa mchanga, udongo na taka ngumu mita 500 juu na chini ili kuruhusu maji yaweze kupita,” amesema Kasekenya.

Aidha, Kasekenya ametoa rai kwa wananchi kuacha kufanya shughuli zao karibu na kingo za mto pamoja na shughuli ambazo zimekuwa zikisababisha maji kushindwa kupita kwenye daraja hilo.

Ameongeza kuwa mazungumzo na Benki ya Dunia ili kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo yanaendelea.

Send this to a friend