Taarifa ya serikali kuhusu ujenzi wa Daraja la Jangwani na Mto Msimbazi

0
34

Serikali imetoa taarifa ya kuhamishwa kwa wakazi wa maeneo ya Bonde la Mto Msimbazi ili kupisha uendelezaji wa mradi katika eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeeleza kuwa lengo kuu la mradi ni kukabiliana na mafuriko na kutumia fursa ya eneo kubwa la wazi litakalopatikana baada ya mradi kukamilika.

“Serikali inapenda kuwajulisha wananchi kuwa hairuhusiwi kufanya uendelezaji wa aina yoyote katika maeneo ambayo tayari yameshatambuliwa na uthamini tangu tarehe 10/11/2021.” OR-TAMISEMI.

Baadhi ya shughuli zitakazotekelezwa na mradi ni pamoja na kuongeza uwezo wa mto kupeleka maji ya mvua baharini kwa haraka, kudhibiti mmomonyoka wa udongo na usimamizi wa taka ngumu, kujenga maeneo ya makazi, biashara na bustani ya jiji pamoja na kujenga daraja la Jangwani.

Ikiwa ni muendelezo wa zoezi la uthamini OR-TAMISEMI inatarajia kufanya uhakiki wa taarifa na mali za wale wanaotegemea kupokea fidia, pia kutafanyika utambuzi wa aina ya fidia wanayopendelea waathirika kati ya fedha taslimu au kufidiwa mali kwa mali.

Send this to a friend