Taarifa ya TACAIDS kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya UKIMWI

0
53

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Hedwiga Swai amesema kwa sasa kuna dawa za UKIMWI ambazo mtu anaweza kutumia kabla ya kufanya tendo la ndoa ili kumkinga na maambukizi.

Utafiti: Hatari inayowakabili walaji wa kuku wa kisasa Dar es Salaam

Amesema hayo wakati TACAIDS ikitoa taarifa yake iliyoonesha kuwa maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI Tanzania yameendelea kupungua hadi kufikia wagonjwa elfu 54 mwaka 2021 kutoka elfu 81 mwaka 2017.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko amesema utafiti uliofanywa umebaini kupungua pia kwa vifo vinavyotokana na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI kutoka watu elfu 32 kwa mwaka 2017 na kufikia elfu 29 mwaka 2021.