Taarifa ya TANAPA kuhusu moto unaowaka Mlima Kilimanjaro

0
40

Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) imesema kuwa moto uliozuka jana eneo la Whona pakupumzikia wageni wanaofanya utalii kwenye Mlima Kilimanjaro unaendelea kudhibitiwa.

TANAPA imebainisha kuwa vikosi vinavyoshirika katika kuudhibiti moto huo vinajumuisha wananchi, wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo na wale wa Chuo cha Mweka na Kikosi cha Zimamoto.

Kuhusu chanzo cha moto huo mamlaka hiyo imesema bado inaendelea kufanyia taarifa mbalimbali ilizozipata.

TANAPA imesema kuwa inaendelea kuchukua tahadhari zote kuhakikisha usalama wa wageni na vifaa vyao unaimarika bila kuathiri shughuli za utalii ambazo zinaendelea kama kawaida hususani kwa njia ya Marangu iliyoathirika na moto huo.

Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu zaidi barani Afrika na mlima mrefu zaidi uliosimama wenyewe duniani.

Send this to a friend