Taarifa ya TANESCO kuhusu kukosekana kwa huduma ya LUKU

0
68

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewatarifu wananchi kuwa watakosa huduma ya LUKU kutokana na kuwepo kwa matengenezo kinga kwenye kanzi data ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wa malipo ya kabla (LUKU).

TANESCO imesema zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Jumatatu Agosti 22 hadi 25 mwaka huu, saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kwa siku nne mfululizo.

Hivyo, TANESCO imewashauri wateja wa huduma hiyo kununua umeme wa ziada au kufanya manunuzi ya umeme nje ya muda huo wa matengenezo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Send this to a friend