Taarifa ya TCRA kwa wote wanaouza na kusajili laini za simu

0
25

Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzaia (TCRA) inaendela na utekelezaji wa zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya biometria, TCRA imebaini kuwa kuna watu wanaojihusisha na usajili wa SIMU bila kuidhinishwa na watoa huduma za mawasiliano.

Kwa mujibu wa kifungu cha 92 na 97 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, 2010 na Kanuni ya 9,10, na 11 ya Kanuni za Usajili wa Laini za Simu (Sim Card Registration Regulations, 2018), TCRA inapenda kuutaarifu na kuukumbusha Umma kuwa:-

  1. Ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kuwa na uthibitisho kuwa ameidhinishwa na mtoa huduma za mawasiliano kutoa huduma hizo;
  2. Yeyote anayejihususha na uuzaji, usambazaji au usajili wa laini za simu anatakiwa kuwa na ofisi ya kutolea huduma hiyo ya usajili wa laini za simu; na
  3. Ni kosa la jinai kwa mtu yeyoye kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kuwa na ofisi na uthibitisho wa idhini ya mtoa huduma husika.

Umma unakumbushwa na kuonywa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani pamoja na faini, kwa mtu yeyote atakaye bainika kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kufuata taratibu.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Jengo la Mawasiliano, Kitalu Na. 20 Barabara ya Sam Nujoma, S. L. P 474, 14414 DAR ES SALAAM JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

Send this to a friend