Taarifa ya TMA kuhusu kuanza mvua za masika

0
45

Mamlaka ya Hali ya Hewa imetangaza taarifa ya utabiri wa hali ya hewa kwa msimu wa mvua za Masika mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Mvua hizo zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza ya Machi 2021 na kuisha katika wiki ya nne ya Mei 2021.

Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa pwani ya Kaskazini.

Mvua katika maeneo hayo zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki ya nne ya Februari 2021 na zinatarajiwa kuisha katika wiki ya tatu ya Mei 2021.

Maeneo mengine ikiwa ni ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Hamza Kabelwa amesema kutokana na mifumo ya hali ya hewa ilivyo kwa sasa na inavyotarajiwa katika kipindi chote cha msimu kwa ujumla mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Send this to a friend