Taarifa ya TMA kuhusu mvua iliyonyesha Dar leo, na utabiri wa kesho

0
25

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua iliyonyesha jijini Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Morogoro, Unguja na Pemba imetokana na mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la Bahari ya Hindi.

TMA imesema mgandamizo huo umesababisha kuvuma kwa upepo wenye unyevunyevu kutoka baharini kuelekea maeneo ya pwani ya nchi.

Mamlaka hiyo imesema mvua hizo ni fupi na kwamba zinatarajiwa kupungua kwa siku ya kesho Oktoba 14, 2020 na kuongezeka kidogo Oktoba 15, 2020.

Aidha, TMA imeeleza kuwa mvua za vuli katika maeneo ya pwani ya Kaskazini na nyanda za juu Kaskazini Mashariki zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Novemba 2020.

Send this to a friend