Taarifa ya TRC kuhusu madai ya mabehewa yake kushikiliwa Ujerumani

0
59

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limekanusha taarifa iliyotolewa katika gazeti la Jamhuri Novemba 22, 2022 yenye kichwa cha habari kilichosomeka ‘Mabewa ya SGR yazuiwa Ujerumani’ na kusema kuwa taarifa hiyo haina ukweli na inapotosha uuma.

TRC imesema mkataba wa matengenezo ya mabehewa 30 na vichwa viwili vya treni kati ya Shirika la Reli Tanzania na kampuni ya Euro Wagon ulivunjwa Februari 2022 baada ya kampuni kushindwa kukidhi matakwa ya mkataba, hatua iliyopelekea TRC kutafuta mkandarasi ambaye ni kampuni ya Lueckemeier Transport and Logistics GMBH ya nchini Ujerumani.

CHADEMA yatishia kutoshiriki uchaguzi mkuu 2025

“TRC haijapokea taarifa yoyote kuhusu kuzuiwa au kuuzwa kwa behewa kutoka kwa mkandarasi ambaye ni kampuni iliyopewa dhamana ya kuendelea na matengenezo ya behewa,” imeeleza taasisi hiyo.

Aidha, imeeleza kuwa kasi ya matengenezo ya behewa bado inaendelea chini ya kampuni ya Lueckemeier Transport and Logistics GMBH.

Send this to a friend