Tabia 5 za mabilionea unazopaswa kuiga mwaka 2022

0
45

1. Wana nidhamu sana na wanafanya kila kitu kulinda ustawi wao wa kimwili na kiakili.

Ni mara chache sana kusikia habari mbaya kuhusu mabilionea barani Afrika, hiyo ni kwa sababu, wengi wao wanajali hadhi yao katika jamii ikiwa ni pamoja na kulinda chapa za biashara zao.

Mabilionea pia wana nidhamu sana linapokuja suala la kutunza afya zao vizuri, na hiyo ni kwa sababu wanajua kwamba utajiri halisi ni afya njema.

2. Ni wazuri sana kwenye kuunda mitandao (connection)

Kuna msemo usemao ‘ndege wa kufanana huruka pamoja.’ Watu matajiri hutengeneza mahusiano na watu wenye hadhi kubwa, hiyo ni kwa sababu huhitaji watu ambao wanaweza kuongeza thamani katika maisha yao kwa njia moja au nyingine.

Mambo matatu ya kufanya unapozimikiwa na gari njiani

3. Mabilionea wanaambatana na watu werevu.

Hatua hii ni sawa na ile iliyo hapo juu, lakini bado ni tofauti. Japokuwa watu matajiri ndio wabeba maono katika biashara zao, bado hawawezi kufanya kazi zote peke yao. Kwa hivyo, hutafuta wataalamu mahiri na wenye elimu ya juu kama vile wanasheria, wahasibu, wataalamu wa mikakati ya biashara,  na wengine ambao watafanya nao kazi kila siku.

4. Wana mikakati mingi  katika harakati zao za biashara.

Linapokuja suala la biashara, mabilionea wanajua kile wanachokitaka na jinsi ya kukipata. Hawaruhusu chochote kizuie mafanikio yao, wanajitahidi kuhakikisha kwamba, hakuna chochote kitakachozuia mafanikio yao.

5. Mabilionea wa Afrika wanasoma sana ili kujifunza mambo mapya na kuelimika zaidi.

Kuna msemo unasema ‘kusoma humjenga mtu’. Kila siku wanakuwa bora zaidi kwa sababu wanayatafuta maarifa. Ikiwa unataka kufanikiwa, amua kujifunza ujuzi mpya na uwe tayari kutumia ujuzi unaoupata kwa manufaa yako.

Send this to a friend