Tabia 6 za kila siku zinasosababisha uwe na kitambi

0
97

Ikiwa utahisi kwamba umeanza kuwa na kitambi, au kitambi chako kinaendelea kukua, huenda hivi karibuni umeanzisha tabia ambazo zinachochea kwa kiasi kikubwa tumbo lako na kuwa na hifadhi kubwa ya nafuta.

Tabia hizo zinaweza kuwa ni pamoja na;

1.Vinywaji vya kaboni

Utafiti umeonesha kuwa, watu wanaokunywa soda kila siku wapo katika hatari mara tano ya kupata vitambi ikilinganishwa na wale ambao hawatumii soda kutokana na kiwango kikubwa cha sukari.

2. Kula usiku sana

Kutokana na majukumu mengi ya kazi, unaweza kujikuta unakula usiku sana na kulala kitandani mara tu unapomaliza kula. Wataalamu wanapendekeza kula chakula cha jioni chepesi na angalau ukae masaa matatu kabla ya kulala.

3. Kutumia sahani kubwa

Utafiti umeonyesha kuwa watu ambao kila wakati hutumia sahani kubwa kila wanapokula, huishia kula sana kwa sababu sahani ina nafasi kubwa, unaweza kuishia kula zaidi ya inavyohitajika. Ikiwa unakula zaidi, basi huwezi kuepuka kupata kitambi.

4. Kunywa pombe kila siku
Pombe imejaa sukari na kalori. Kalori hizi zote zitajikusanya kwenye tumbo lako na matokeo yake tumbo lako litakuwa kubwa.

5. Kutofanya mazoezi

Kwa wastani, tunatumia saa nane kulala, na karibu saa nane zaidi kazini. Hiyo inamaanisha kwamba miili yetu haifanyi kazi mara nyingi na hii inasababisha mkusanyiko wa mafuta karibu na matumbo yetu. Ikiwa kazi yako haihusishi kuzunguka, basi lazima ufanye mazoezi mara kwa mara ili kuepuka mafuta ya tumbo.

6.Kula wakati una hisia mbaya

Unapokuwa na hasira au huzuni sio wakati mzuri wa kuvamia friji yako na kula chochote unachopata. Watu wengine hujaribu kutuliza hisia zao kwa kula chakula kisicho na afya na kuishia kula hovyo bila kufikiria afya zao.