Tabora United yafungiwa kufanya usajili wa wachezaji

0
107

Klabu ya Ligi Kuu ya NBC ya Tabora United ambayo ilikuwa ikiitwa Kitayosce FC imefungiwa kufanya usajili wa wachezaji wa kimataifa mpaka itakapomlipa mchezaji Asante Kwasi.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo raia wa Ghana kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo akidai malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mshahara.

“Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo,” imesema taarifa iliyotolewa na TFF.

Rais Samia aipa Twiga Stars milioni 10

Mbali na uamuzi huo wa FIFA kuifungia klabu hiyo kufanya usajili, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa ndani.