Tabora United yafungiwa na FIFA

0
14

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia klabu ya Tabora United kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake, Evariste Kayembe.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema uamuzi huo umefanywa baada ya mchezaji huyo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kushinda kesi ya madai dhidi ya Tabora United aliyoifungua FIFA akidai malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mishahara.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa, Tabora United ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini hukumu hiyo haikutekelezwa.

Hata hivyo, baada ya uamuzi wa FIFA kuifungia kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa TFF imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa ndani huku ikizikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.