Tahadhari Homa ya Mgunda kwa walaji wa nyama choma

0
16

Wizara ya Afya imetoa tahadhari kwa walaji wa nyama choma ‘mishikaki’ kuhakikisha kuwa nyama zinaiva vizuri ili kuepukana na hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mgunda.

Hayo yameelezwa na mtaalam wa afya ya jamii kutoka wizara hiyo, Dkt. Azma Simba ambapo amewataka wananchi kuchukua tahadhari wakati Serikali ikiendelea kutoa elimu kwa wananchi wa mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

“Kwa wale watumiaji wa mishikaki au nyama choma yoyote wahakikishe kuwa vyanzo vyao ni salama, na nyama ile inakuwa imekaguliwa ili kuepusha madhara ya kiafya ikiwemo homa ya mgunda na magonjwa yoyote yanayoambukizwa na wanyama,” amesema Dkt. Simba.

Takribani wagonjwa 20 wameripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo, huku watu watatu wakithibitika kufariki katika halmashauri ya Ruangwa mkoa wa Lindi.

Send this to a friend