Tahadhari kwa wanawake wanaotumia dawa za kusimamisha matiti

0
105

Madaktari wameonya matumizi holela ya dawa za kusimamisha matiti kwa wanawake kwa kuwa dawa hizo zinamuweka mtu katika hatari ya kupata magonjwa.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Dkt. Samwel Shitta amewaonya wanawake wanaotumia dawa hizo hasa zinazouzwa mitandaoni kwa kuwa hazijulikani zimetengenezwa kwa kutumia kemikali zipi ambazo zikiingia ndani ya seli zinafanya kazi gani mwilini.

“Dawa za mitandaoni hazijatafitiwa kujua madhara yake ni yapi endapo mtu atatumia, hii ni tofauti na dawa za hospitali ambazo kabla ya kuwa pale zimetafitiwa na kuona madhara ambayo mtu anaweza kupata akitumia,” ameeleza.

Dkt. Shitta amesema wafanyabiashara wanaouza dawa hizo mitandaoni wanatumia maneno mazuri yanayowashawishi watu kununua bidhaa hizo bila kuwaambia madhara yanayoweza kutokea baada ya matumizi.