TAKUKURU yabaini watumishi wawili Arusha wameghushi nyaraka

0
16

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha imebaini watumishi wawili kuhusika kughushi nyaraka ikiwemo kutengeneza namba bandia ya mlipakodi na kutumia kampuni hewa kulipia mapato.

Uchunguzi huo umefanyika ikiwa ni agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kufuatia tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo kudai kulipa kodi ya huduma TZS milioni 24 lakini akapewa risiti ya TZS milioni 3.6.

TAKUKURU imesema kwa sasa inafanya uchunguzi wa mfumo mzima wa malipo ili kubaini kampuni nyingine hewa na namba bandia za mlipakodi zilizotumika kuchepusha kodi au mapato yoyote katika halmashauri hiyo.

“Uchunguzi kwa sasa uko juu ya watumishi wawili, mmoja tumebaini ndiye aliyetengeneza namba bandia ya mlipakodi na mwingine anaweza kampuni hewa ya kulipia makusanyo, tunaendelea na uchunguzi ili kubaini kuna kitu kinaweza kusababisha ubadhilifu,” ameeleza Mkuu wa TAKUKURU mkoani Arusha, Zawadi Ngailo katika mahojiano na Mwananchi.

Send this to a friend