TAKUKURU yaeleza sababu ya matukio ya rushwa ya ngono kuwa siri

0
50

Taasisi ya Kuzua na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Simiyu imesema watu wengi hawaripoti matukio ya rushwa ya ngono katika ofisi zao au mamlaka nyingine kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Janeth Machulya ambapo ameeleza kuwa licha ya ofisi yake kutopokea taarifa hata moja ya rushwa ya ngono, bado kumekuwa na taarifa za pembeni za matukio hayo ambazo wamekuwa wakizisikia kutoka kwa wananchi.

Hata hivyo Machulya ameongeza kuwa katika kupambana na hilo hivi karibuni waliandaa warsha na wadau wa elimu kuchambua mifumo ya viashiria vya rushwa, kisha waliazimia kuunda madawati ya rushwa ya ngono kwa ajili ya kuripoti matukio hayo.

“Jambo ambalo tumeligundua ni kuwa rushwa ya ngono kuigundua ni kazi ngumu sana, kwani kuna usiri mkubwa sana lakini pia wengi hawana ujasiri wa kuripoti haya matukio, ndiyo tukaja na hiyo njia ya madawati ambayo watu wanaweza kuyatumia kutoa taarifa,” amesesema Machulya

Send this to a friend