Takwimu: Wanawake wanaongoza kuuliwa na wenza wao

0
65

Kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC) kimesema takwimu zinaonesha kwa mwaka 2021 matukio ya mauaji kwa wenza, wanawake wanaongoza kuuliwa kwa asilimia 89 zaidi ya wanaume.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga amesema kati ya matukio 35 ya mauaji yaliyoripotiwa, wanawake walikuwa 31, huku wanaume wakiwa wanne.

Aidha, ameongeza kuwa katika matukio 111,152 ya mwaka 2019, 2020 na 2021, wanawake walikuwa 66,139 ambayo ni sawa na asilimia 60.

Dada wa kazi amnyonga mtoto siku mbili baada ya kuajiriwa

“Ndani ya mwezi Mei pekee, LHRC imepokea visa saba vya mauaji ya wenza yatokanayo na wivu wa mapenzi ikiwemo tukio lililotokea jijini Mwanza hivi karibuni,” amesema Henga

Hata hivyo, amesema chanzo cha wivu wa mapenzi kinatokana na migogoro ndani ya ndoa licha ya kuwepo chombo cha usuluhishi wa migogoro ya ndoa kabla ya mahakama kutoa talaka.