Takwimu za wagonjwa wa corona waliopo Tanzania hadi leo Mei 17

0
46

Rais wa Tanzania, Dkt Magufuli amesema kuwa hali ya maambukizi ya virusi vya corona nchini imeanza kupungua na hivyo kupelekea baadhi ya hospitali au vitu vya kuwahudumia kubaki vitupu.

Ameyasema hayo Mei 17, 2020 wakati akitoa salamu kwa Watanzania katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chato, mkoani Geita aliposali ibada ya Jumapili.

“Mimi namwamini Mungu na Mungu amejibu maombi yetu, tumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutusikiliza na tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu wa Corona” amesisitiza Rais Magufuli.

Takwimu alizotoa zinaonesha kuwa mpaka leo (17 Mei, 2020) Hospitali ya Amana (Dar es Salaam) iliyokuwa na wagonjwa 198 imebakiwa na mgonjwa 12, Hospitali ya Mloganzila iliyokuwa na wagonjwa 30 imebakiwa na wagonjwa 6, Kituo cha Lulanzi (Kibaha) kulikuwa na wagonjwa zaidi ya 50 wamebaki 22.

Vituo vingine ni Agha Khan ambapo wamebaki wagonjwa 31, Hindu Mandal 16, Regency wamebaki 17, TMJ 7, Rabinisia 14, Moshono (Arusha) 11, Longido 0, Karatu 0, Buswelu 2, Misungwi 2, Ukerewe 0, Magu 0, Mkuyuni 0, Nyahunge 0, Sengerema 0.

Takwimu pia zinaonesha Kwimba 0, Bugando na Sekou Toure 2, Dodoma 2 (kutoka zaidi ya 40), Kongwa 0, Kondoa 0 nakadhalika. Na kwamba wagonjwa wengi wana hali nzuri.

Amesisitiza kuwa viongozi na Watanzania wote wasiwe na hofu kubwa dhidi ya ugonjwa wa Corona kiasi cha kusababisha matatizo mengine ikiwemo kutowahudumia ipasavyo wagonjwa mbalimbali ambao baadhi wanaambiwa wana Corona ilihali hawajaambukizwa ugonjwa huo.

Send this to a friend