Takwimu zaonesha wanawake wanaongoza matumizi ya dawa za kulevya

0
56

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limesema idadi ya wanawake wanaotumia dawa za kulevya mkoani humo inaongezeka zaidi ikilinganishwa na idadi ya wanaume.

Ameyasema hayo mratibu wa Jeshi la Polisi kutoka Ofisi ya ushirikishwaji wa jamii wa Jeshi, Denis Rwiza wakati akisoma taarifa ya mwenendo wa vitendo vya matumizi ya dawa za kulevya mkoani Mwanza katika utangulizi wa siku ya kupambana na Dawa za kulevya.

Amesema kati ya Februari hadi Mei mwaka huu idadi ya wanaume waliokamatwa kwa matumizi ya dawa za kulevya ni 132 kulinganishwa na mwaka jana walikuwa 174, huku idadi ya wanawake kwa mwaka huu wakiwa 22 wakati mwaka jana walikuwa 10.

Serikali kuongeza kima cha chini cha mishahara Sekta binafsi

“Kwa hiyo kuna ongezeko la watu 12 huku wanaume idadi ikipungua kwa watumiaji 42”, amesema.

Maadhimisho ya siku ya kupambana na dawa za kulevya unatarajiwa kufanyika kitaifa Julai 02 jijini Dar es Salaam ikibeba kaulimbiu isemayo ”Tukabiliane na dawa za kulevya kwa Ustawi wa Jamii.”

Send this to a friend