Talaka tano zilizogharimu fedha nyingi zaidi duniani

0
38

Mei 3 mwaka huu, bilionea Bill Gates ameingia katika kitabu cha historia baada ya kutangaza kuwa yeye na mkewe, Melinda Gates wamefikia makubaliano ya kuvunja ndoa yao iliyodumu kwa miaka 27.

Bill Gates ambaye kwa mujibu wa Forbes ni tajiri namba nne dunia akiwa na utajiri wenye thamani ya TZS trilioni 287.6 ataendelea kushirikiana na Melinda Gates kupitia Bill & Melinda Gates Foundation, taasisi ambayo inalenga kuisaidia jamii katika masuala ya afya, elimu na usawa wa kijinsia.

Hatua hii inafuata miaka michache baada ya bilionea Jeff Bezos kutalikiana na mkewe. Lakini je, unazijua talaka tano zilizogharimu fedha nyingi zaidi, makala hii inazileta kwako;

  1. Jeff na MacKenzie Bezos- TZS trilioni 81.2
    Waanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos na mkewe MacKenzie walitalikiana Aprili 4, 2019 baada ya miaka 25 ya ndoa yao. Kutokana na talaka hiyo, Mackenzie alipewa asilimia 4 ya hisa za Amazon, ambazo zilikuwa na thamani ya TZS trilioni 81.2

Kutokana na thamani hiyo ya talaka yake, kwa wakati huo alitarajiwa kuwa atakuwa mwanamke wa tatu kwa utajiri duniani.

  1. Bill na Sue Gross- TZS Trilioni 3.01
    Sue alidai talaka mwaka 2016 kutoka kwa mumewe, mwanzilishi wa Pimco na mwaka mmoja baadaye alifanikiwa kuondoka na TZS trilioni 3.01

Kutokana na gharama za talaka hiyo, Bill alipoteza nafasi yake katika orodha ya The Forbes 400 mwaka 2018, baada ya kuwepo kwenye orodha hiyo kwa miaka 14 mfululizo.

  1. Steve na Elaine Wynn- TZS trilioni 1.97
    Mwanzilishi mwenza wa Wynn Resorts alitalikiwa (kwa mara ya pili) mwaka 2010. Kwa talaka hiyo, Elaine ambaye alikuwa mjumbe wa bodi ya Wynn Resorts tangu mwaka 2002 alipokea hisa milioni 11 ambazo kwa wakati huo zilikuwa na thamani ya TZS trilioni 1.8.

Mbali na hilo, Steve aliuza hisa zenye thamani ya TZS bilioni 264.4, fedha ambazo sehemu yake pia zilikwenda kwa Elaine kama sehemu ya makubaliano yao.

  1. Harold Hamm na Sue Ann Arnall- TZS Trilioni 2.3
    Baada ya miaka kadhaa ya mvutano makahamani, tajiri wa mafuta Harold mwaka 2015 aliivunja ndoa yake iliyodumu kwa miaka 26 kwa kumwandikia cheki yenye thamani ya TZS trilioni 2.3.

Baadaye Sue alikwenda makamani akitaka kulipwa TZS trilioni 31.8 lakini hakufanikiwa.

  1. Roy E. na Patricia Disney- TZS Trilioni 1.4
    Baada ya miaka 52 ya ndoa, wawili hao walifungua maombi ya talaka mwaka 2007 wakiwa na miaka 77 na 72, mtawalia. Kwa wakati huo Roy alikuwa na utajiri wenye thamani ya TZS trilioni 3.01, ambapo alipoteza takribani nusu ya utajiri wake katika kutalikiana huko.

Swali linabaki, Bill Gates na Melinda wataingia katika orodha hii ya mabilioni waliotema fedha nyingi zaidi katika talaka zao?

Send this to a friend