Taliban yapiga marufuku TikTok, yaeleza sababu

0
29

Baada ya hivi karibuni kundi la Taliban kupiga marufuku muziki, sinema na michezo ya kuigiza ya televisheni, kundi hilo limetoa sharti jingine kali la kuzuia mtandao wa video wa TikTok na mchezo wa mtandaoni wa PUBG kutumika nchini Afghanistan.

Kundi la wanamgambo hao lilitoa sababu za kufanya hivyo likidai kuwa programu hizo zinasababisha vijana wa Afghanistan kupotea.

Aidha, wameendelea kutishia kupiga marufuku vituo vya televisheni kurusha hewani kile walichokiona kuwa ‘vitu visivyo vya maadili’ na msemaji wa Taliban alisema kuwa, wanafanya hivyo ili kuzuia kizazi kipya kupotoshwa.

Kundi laTaliban liliahidi uhuru lilipochukua mamlaka mwaka jana lakini inatafsiriwa kuwa kinyume chake na kuwakandamiza zaidi wananchi hasa wanawake.

Idadi ya watumiaji wa mtandao nchini Afghanistan, imeongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni wakifika takribani milioni tisa hivi sasa.

Send this to a friend