TAMISEMI yaongeza siku 9 za kupokea maombi ya ajira za ualimu
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeongeza muda wa siku tosa wa kupokea maombi ya nafasi za ajira ya walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka Septemba 21hadi Septemba 30 mwaka huu.
TAMISEMI imechukua hatua hiyo ili kufidia kipindi ambacho kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa mtandao katika mfumo wa maombi ya ajira ya walimu.
Mamlaka hiyo imesema kuwa changamoto hizo zimetatuliwa na mfumo wa maombi ya ajira ya walimu umeongezewa uwezo na unapatikana kwa urahisi zaidi hivyo wenye sifa wanaweza kuendelea kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha https://ajira.tamisemi.go.tz (Online Teacher Employment Application System – OTEAS).
Septemba 7 mwaka huu TAMISEMI ilitangaza nafasi hizo za ajira ambapo awali mwisho wa kupokea maombi ilikuwa ni leo Septemba 21, 2020.
Hapa chini ni tangazo la nafasi hizo ambalo linaelezea sifa za wanaotakiwa kutuma maombo;