Tamko la TRC ajali ya treni Tabora

0
80

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema ajali ya treni iliyotokea leo Juni 22, eneo la Malolo mkoani Tabora imesababisha jumla ya vifo vinne wakiwemo watoto wawili pamoja na majeruhi 132.

Treni hiyo ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Kigoma kuelekea Dar es salaam ilipata ajali majira ya saa 11 asubuhi ikiwa na behewa nane zilizokuwa na abiria 930.

Taarifa inasema treni ilipofika eneo la Malolo (Kilometa 10 kutoka stesheni ya Tabora) behewa tano za abiria daraja la tatu, behewa moja la vifurushi, behewa moja la huduma ya chakula na vinywaji pamoja na behewa la breki zilianguka na kusababisha ajali.

Aidha Shirika limesema linaendelea na zoezi la kuwasafirisha manusura wa ajali hiyo kutoka Tabora ili kuendelea na safari ya kuelekea Dar es salaam, pamoja na kufuatilia chanzo cha ajali.

Send this to a friend