TANAPA yakanusha kujenga lami Hifadhi ya Serengeti

0
72

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania  (TANAPA) limesema maboresho ya teknolojia yanayokusudiwa kufanywa ndani ya hifadhi hayahusishi matumizi ya lami.

Taarifa hiyo iliyotolewa na TANAPA imefuatia baada ya moja ya chombo cha habari kuripoti kuwa ‘Serengeti sasa kujenga lami hifadhini’ ambapo imesema ni kweli ipo katika harakati za kujaribu matumizi ya teknolojia yatakayoboresha barabara hifadhini lakini si kujenga lami katika hifadhi.

Rais afanya uteuzi mpya, Mchechu ateuliwa Hazina, Makame NHC

“Ni kweli kwamba TANAPA iko katika harakati za kujaribu matumizi ya teknolojia mbalimbali zitakazowezesha kuboresha barabara kwenye hifadhi za taifa hususani Hifadhi ya Taifa Serengeti ili kupunguza changamoto na malalamiko mengi toka kwa watumiaji wake,” imesema TANAPA.

Aidha, TANAPA imesema nia yao ni kulenga kwenye teknolojia ambayo itakuwa endelevu na rafiki kwa mazingira kwenye Hifadhi za Taifa na si vinginevyo kama ilivyoelezwa.

Send this to a friend