TANAPA yatangaza gharama ya milioni 5 kwa anayetaka kumpa mnyama jina

0
56

Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) imesema imeanzisha programu ya kuwapa majina baadhi ya wanyama waliopo kwenye Hifadhi za Taifa kwa yeyote ayakayevutiwa kufanya hivyo.

Akizungumza Kamishna wa uhifadhi TANAPA, William Mwakilema amesema mtu atakapohitaji mnyama apewe jina lake atatakiwa alipie kiasi cha TZS  milioni 5 na TZS milioni 1 kila mwaka kwa yeyote ambaye angependa kumuasili na kumtembelea kila mwaka.

Waziri Mkuu atoa siku saba TARURA, DAWASA kukamilisha barabara ya Muhimbili

“Kumuasili yaani umemu-adopt, una interest, kila mwaka unataka umuone na wewe kama Mtanzania yaani una uchungu na hawa wanyama wasije wakatoweka, kila mwaka unalipa hiyo milioni moja ambayo inaendelea kuchangia gharama za kumhifadhi yule mnyama,” amesema.

Aidha, amesema TANAPA imeanza na baadhi ya wanyama ambao ni Faru na tayari utaratibu huo umepitishwa na menejimenti kwa yeyote atakayevutiwa kufanya hivyo.

Send this to a friend