TANESCO: Hatuhusiki na kukatika umeme ndani ya Bunge

0
12

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limefafanua kuwa tatizo la kukatika kwa umeme leo wakati kikao cha bunge hakuhusiani na laini ya yake inayopeleka umeme bungeni.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Martin Mwambene amesema laini ya umeme ya Bunge inaangaliwa kwa makini kwa kuwa hiyo ni taasisi nyeti na inapewa kipaumbele kama ilivyo kwa hospitali.

“Tumeona hiyo taarifa kwamba kuna tatizo la umeme lakini tunaamini tatizo halitoki kwetu na laini yetu haijaharibika,” amesema.

Mwambene ameongeza kuwa watu wamekuwa wakihusisha kila kukatika kwa umeme na TANESCO, jambo ambalo siyo kweli kwani wajibu wa TANESCO unaishia kwenye mita, na kwamba ukiingia ndani, ni eneo linalomhusu mteja.

TRA: Ukamataji unafanyika tunapofanya ukaguzi kujiridhisha

“Tatizo ambalo limepatikana hapo [bungeni] halihusiani na laini yetu kutoka au vinginevyo, na kuzima na kuwaka ni dalili pia ya shoti, sasa shoti inaweza kuwa ndani ya majengo yenyewe au vinginevyo,” ameongeza Mwambene.

Katika kikao cha bunge mapema leo Mei 15, 2023 Spika Dkt. Tulia Ackson alisitisha kikao hadi saa 10 jioni kutokana na hitilafu ya umeme ambao ulikatika mara mbili ndani ya muda mfupi.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend