TANESCO: Kukosekana kwa umeme katika mikoa 14

0
77

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kukosekana kwa huduma ya umeme katika baadhi ya mikoa 14 nchi nzima kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye moja ya mitambo ya kuzalishia umeme kwenye bwawa la Mtera.

TANESCO imesema hitilafu hiyo imesababisha upungufu wa uzalishaji umeme hivyo kupelekea kukosekana kwa huduma ya umeme katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Iringa, Manyara, Singida, Geita, Arusha, Morogoro, Shinyanga, Njombe, Tanga, Pwani na Dar es salaam.

“Wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kuhakikisha huduma ya umeme inarejea kwa wateja wote na tutawataarifa huduma itakaporejea, Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote ule unaojitokeza” imeandika TANESCO.