TANESCO: Matengenezo ya mitambo na ukame chanzo cha upungufu wa umeme

0
15

Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande amesema kuwa shirika hilo inapita kipindi kigumu cha upungufu wa umeme unaosababishwa na ukame na matengenezo ya mitambo, ambapo upungufu uliopo ni megawati 300MW – 350MW.

Ametaja vituo vilivyoathiriwa zaidi na ukame kuwa ni Kihansi (17MW vs 180MW, 163 hauzalishwi), Pangani (10MW vs 68MW, 58 hauzalishwi), Mtera (175MW vs 180MW, 5 hauzalishwi), Nyumba ya Mungu (3MW vs 8MW, 5 hauzalishwi).

Vituo vilivyo kwenye Matengenezo Kidatu (150MW vs 200MW, 50 hauzalishwi), Ubungo III (32MW vs 112MW, 80 hauzalishwi), Kinyerezi II(195MW vs 248MW, 53 hauzalishwi), hivyo kufanya jumla ya umeme ambao hauzalishwi kwa sababu ya ukame na matengenezo kuwa ni 414MW.

Ametaja hatua za muda mfupi za kukabiliana na tatizo kuwa ni kuharakisha matengenezo ya mitambo hiyo ambapo inatarajiwa 90MW zitapatikana kama ifuatavyo:

a. Mashine moja ya 40MW ya Ubungo III , kurudi tarehe 25.11.2022.
b. Mashine ya Kidatu 50MW kurudi 28.11.2022.
c. Mashine mbili za Ubungo III 40MW kurudi kabla ya mwisho wa Disemba.
d. Kupatikana mashine mpya ya Kinyerezi I 90MW kabla ya mwisho wa Disemba.

“Kama ukarabati ukikamilika kama ulivyopangwa itatupatia 220MW kwenye uzalishaji na kupunguza kadhia hii ya umeme. Mipango ya muda wa kati ambayo itapatikana mwezi Februari ni mashine nyingine ya 90MW itaanza kuzalisha umeme na kufikisha jumla ya 310MW,” amesema.

Ameongeza kuwa kwa kipindi hiki mvua zikipatikana hali ya umeme itaimarika mapema zaidi, na kama hakutakuwa na hitilafu nyingine itakayo jitokeza.

Ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi za kinachoendelea TANESCO hutoa taarifa kila wiki kwa kukutana na waandishi wa habari na kila siku katika tovuti ya club house.

Send this to a friend