TANESCO: Upatikanaji umeme utaimarika Desemba 2022

0
50

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kutokana na ukame mkubwa ulioikumba nchi, uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji umepungua kwa jumla ya megawati 155 za umeme hali iliyochangiwa na mabwawa ya kufua umeme ya Kihansi, Mtera, Nyumba ya Mungu, Hale na Pangani kupungua uzalishaji umeme.

Imeeleza kuwa mtambo mmoja wa Kidatu unaozalisha Megawati 50 umepata hitilafu na mitambo miwili ya Ubungo III inayozalisha megawati 40 ipo kwenye matengenezo kinga, hivyo kupunguza takribani megawati 300 za umeme wa maji na gesi.

Hali hiyo itadumu hadi mwanzoni mwa mwezi Desemba 2022 baada ya kumalizika matengenezo na kuongezeka maji kwenye mabwawa pamoja kuingizwa megawati 225 kwenye Gridi ya Taifa.

Aidha, TANESCO imesema ifikapo mwishoni mwa Desemba, 2022 inategemea kupata megawati 65 kupitia Kinyerezi I, megawati 45 na Ubungo III, megawati 20 na kufanya jumla ya megawati 225 za umeme kurudi kwenye Gridi ya Taifa na kupunguza upungufu wa umeme.

Send this to a friend