TANESCO yaagizwa kutokata umeme kipindi chote cha uchaguzi
Waziri a Nishati Dkt. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha umeme haukatiki katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu hususani siku ya kupiga kura.
“Maeneo yote kuanzia kwenye vijiji, kata wilaya na mikoa nchi nzima umeme usikatike wakati wa uchaguzi, usikatike maeneo yote na muda wote lakini hasa hasa wakati wa kupiga kura tarehe 28, Oktoba, tunataka wananchi wapige kura kwa uhuru na
uhakika.”
Ametoa agizo hilo alipotembelea kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Dege, na kuongeza kuwa ujenzi wake umefikia asilimia 81 na amewaagiza wakandarasi kuhakikisha ifikapo Novemba 2020 ujenzi uwe umekamilika kwa asilimia 100.
“Niwapongeze TANESCO na mkandarasi kwa hatua mliyofikia ingawa mkandarasi aliomba miezi
miwili kukamilisha kazi hii mimi nimesema hapana, kwanza kazi yenyewe iliyobaki ni ndogo hivyo nimetoa mwezi mmoja kufikia Novemba ujenzi uwe umekamilika,” amesisitiza Dkt. KJalemani.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Meneja Mradi, Mhandisi Neema Mushi ameema mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 26. 2 ikijumuisha na ulipaji fidia kwa wakazi waliohamishwa kupisha mradi.