TANESCO yatangaza mikoa 17 itakayokosa umeme kwa saa 10

0
64

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kukosekana kwa umeme kwenye baadhi ya maeneo nchini kuanzia Jumapili Oktoba 09 hadi Jumatatu Oktoba 10, 2022.

Shirika limesema sababu ni kuzimwa kwa laini mbili kubwa za umeme (Kilovoti 220) kutoka Morogoro hadi Kinyerezi na Morogoro hadi Kidatu.

Baadhi ya maeneo yatakayoathirika ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Arusha, Morogoro, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Njombe, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mara, Simiyu, Kilimanjaro, Manyara na Songwe.

Muda wa kukatika kwa umeme kwa Oktoba 9 ni Saa 1 na nusu asubuhi hadi saa 10 na nusu jioni, na Saa 1 na nusu asubuhi hadi 9 na nusu alasiri kwa Oktoba 10, 2022.

Send this to a friend