Tanga: Mtoto wa miaka 9 akamatwa kwa tuhuma za kumuua mwenzake mwenye miaka 9

0
55

Jeshi la polisi mkoani Tanga linamshilikia mtoto (9), mkazi wa Mji Mpya Hale, wilayani Korogwe ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kichangani kwa tuhuma za mauaji ya Ally Khalifa Bakari (9), mwanafunzi wa darasa la tatu shule hapo, na mkazi wa Msalo Hale.

Akizungumza na TBC Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema mauaji hayo yametokea majira ya saa nane Januari 28 mara baada ya wanafunzi hao kutoka Msikitini.

Amesema tayari maafisa wa polisi wakiongozwa na mkuu wa upelelezi wilayani Korogwe wamefika katika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Jongo amesema mwili wa marehemu umekutwa na majeraha mengi sehemu mbalimbali hivyo uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini kama tukio hilo limefanywa na mwanafunzi huyo pekee.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu, Riziki Selungato amesema watoto hao waliruhusiwa muda wa saa sita na robo mchana ili waende Msikitini kuswali wakiwa salama.

Chanzo: TBC

Send this to a friend