Tangazo la nafasi za kazi Yanga SC

0
57

Klabu ya Yanga imewatangazia wanachama wake nafasi za ajira katika nafasi zifuatazo:

1. Mtendaji Mkuu (Chief Executive Officer)

2. Mkurugenzi wa Fedha (Director of Finance)

3. Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano.

4. Meneja Mahusiano (Relationship Manager)

5. Afisa Rasilimali watu (Human Resource Officer)

6. Afisa Habari (Information Officer).

7. Meneja wa Miradi (Project Manager).

8. Msaidizi wa Ofisi ya Mtendaji Mkuu (Personal Assistant to the Chief Executive Officer).

9. Daktari wa timu (Orthopaedist).

Sifa za mwombaji:
• Muombaji lazima awe Mwanachama hai wa Yanga

• Kwa nafasi ya Mtendaji Mkuu, Mkurugenzi na Meneja lazima awe na elimu angalau ya Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu chochote kinachotambuliwa na mamlaka za vyuo vikuu Tanzania.

• Kwa nafasi ya Mtendaji Mkuu na Meneja awe amewahi kuwa Afisa Mwandamizi kwa kipindi kisichopungua miaka mitano (5)

• Kwa nafasi nyingine lazima awe na elimu ya diploma

• Awe na uzoefu wa uongozi wa mpira kwa ngazi za juu kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu (3)

• Asiwe amewahi kukutwa na hatia ya makosa ya jinai

Jinsi ya kutuma maombi;
• Barua ya maombi iambatanishwe na wasifu (resume), nakala ya kadi ya uanachama, nakala ya cheti cha elimu ya chuo kikuu, nakala ya cheti cha kidato cha nne. Nakala hizo zithibitishwe na muhuri wa mwanasheria.

• Barua ya tawi husika ya mwombaji kuthibitisha uanachama wake.

• Mwombaji lazima aambatanishe barua ya Serikali ya mtaa anapoishi (scanned copy)

• Maombi lazima yawe na mawasiliano ya barua pepe na namba za simu za muombaji.

• Nafasi hizi ni kwa wanachama wa Yanga tu si vinginevyo.

• Wanawake watapewa vipaumbele.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18/08/2022 saa kumi kamili jioni.
Maombi (na viambatanisho/attachments) yatumwe kwa njia ya barua pepe kupitia; Email: Info@yangasc.africa.

Send this to a friend