Tani 1,000 za sukari isiyofaa kwa matumizi yaingizwa sokoni Kenya

0
34

Mdhibiti Mkuu wa Shirika la Viwango vya Kenya (KEBS) na maafisa wengine 26 wa serikali nchini Kenya wamesimamishwa kazi kutokana na kuingizwa sokoni tani 1,000 za sukari isiyofaa kwa matumizi ya binadamu.

Uchunguzi wa vyombo vya usalama unasema kuwa sukari iliyopakiwa katika mifuko 20,000 yenye kilo 50 iliingizwa nchini humo Juni 2018 na kampuni ya Merako Investments Limited kutoka Harare, Zimbabwe.

Baada ya kutia nanga katika Bandari ya Mombasa, sukari hiyo ilichakatwa na maafisa wa Shirika la Viwango la Kenya (KEBS) na kuthibitishwa kutofuata viwango vya ubora vya Kenya hivyo kukataliwa kwa matumizi ya binadamu na kutengwa kwa ajili ya kuharibiwa kwa kubadilishwa kuwa ethanoli ya viwandani.

Mwongozo wa KEBS unasema kuwa bidhaa ambazo hazifuati viwango vya ubora wa ndani hazifai kuruhusiwa kuingia nchini na zinapaswa kusafirishwa tena, kurejeshwa au kuharibiwa kwa gharama ya mwagizaji.

Usitishwaji huo unakuja wakati Wakenya wakikabiliwa na ongezeko kubwa la bei ya bidhaa ikiwemo sukari kwa miaka mingi huku kukiwa na uhaba wa bidhaa hiyo nchini humo.

Send this to a friend