Tanzania, Burundi, na DRC zasaini makubaliano ya ujenzi wa SGR

0
41

Tanzania, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jana Jumanne Disemba 3, 2019 zilisaini makubaliano ya kujenga reli ya kisasa (SGR) itakayounganisha nchi hizo tatu, kwa lengo la kurahisishsa usafiri.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema reli hiyo itaziunganisha nchi hizo mbili na Bandari ya Dar es Salaam.

Amebainisha pia kuwa upembuzi yakinifu unaofanywa na Kampuni ya HP Gulf kutoka Ujerumani utakamilika mwishoni mwa Januari 2020. Hata hivyo Waziri Isack Kamwelwe hakubainisha chanzo cha mapato cha ujenzi wa reli hiyo.

Novemba mwaka huu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kuwa Tanzania na Rwanda zipo katika hatua za mwisho za kukamilisha majadiliano kuhusu ujenzi wa SGR kutoka Bandari Kavu ya Isaka nchini Tanzania hadi Rwanda.

Alisema kuwa tayari upembuzi yakinifu wa kipande hicho cha reli ulisha kamilika na kwamba nchi hizo sasa zinatafuta fedha kwa ajili ya kufadhili ujenzi huo.

Send this to a friend