Tanzania, Hungary kukuza ushirikiano kwenye elimu na uwekezaji

0
40

Tanzania imetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kutoka nchini Hungary kusoma kwenye vyuo vikuu vya Tanzania ambapo kwa kuanzia ufadhili huo utaanza na wanafunzi watano.

Hayo yamesemwa leo Julai 18, 2023 wakati Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Hungary, Katalin Novak wakizungumza na vyombo vya Habari mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano katika elimu ambayo yamefaanywa na Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda na Waziri wa Nchi wa Hungury, Tristant Azbej.

Katika kikao hicho, Rais Samia amesema Tanzania na Hungary zimekubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kukuza uwekezaji baina ya nchi hizo pamoja na kuhimiza wawekezaji kutoka Hungary kuwekeza katika maeneo ya kimkakati kama vile nishati jadidifu, utalii, madini, viwanda na uvuvi na pia kuwakaribisha raia wa Hungary kuja kuwekeza nchini.

“Tanzania na Hungary wamekuwa wakishirikiana vizuri katika sekta ya utalii. Tanzania ilipokea watalii 7,188 kutoka Hungary mwaka 2022 [..] ingawa idadi hiyo si kubwa sana, lakini ndio watalii wengi zaidi kuwahi kurekodiwa nchini kutoka Hungary,” amesema.

Kwa upande wa Rais Katalin, amesema ushirikiano baina ya nchi yake na Tanzania umekuwa na manufaa makubwa kutokana na kila nchi kushirikiana na nyingine katika maendeleo.

Ameongeza kuwa nchi yake iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali hasa yanayohusu uongozi na kuwawezesha wanawake kiuchumi na katika ngazi za uongozi

Send this to a friend