Tanzania imevuka wastani wa unywaji pombe Afrika

0
70

Serikali imesema takwimu zinaonesha Tanzania inaongoza kwa matumizi ya unywaji pombe barani Afrika huku watu wenye umri wa kuanzia miaka 15 wakitumia wastani wa ndoo moja ndogo kwa mwaka.

Akizungumza Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasiyoambukiza (NCD) kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Omary Ubuguyu amesema matumizi ya pombe ni chanzo kikuu cha magonjwa yasiyoambukiza na kubainisha kuwa kwa mwaka 2012 asilimia 29 ya Watanzania walikuwa wanakunywa pombe huku zaidi ya asilimia 24 wakiwa ni wanaume.

“Hiki si kipimo kikubwa cha pombe. Kipimo kikubwa ni kwa kiwango gani taifa hili linatumia pombe ili kusema matumizi ni kiwango cha kawaida au kiwango kilichokithiri.

Utafiti: Asilimia 63 ya Watanzania wanafurahia Serikali inavyosimamia uchumi

Kwa Tanzania ukiangalia takwimu, hata juzi zilitoka kwamba inongoza Afrika. Kwa wastani, kiwango cha unywaji kwa mwaka ni lita 9.1 (sawa na ndoo ndogo ya lita 10) wakati kiwango kwa Afrika ni lita sita. Sisi tuko juu kwa lita 3.1 zaidi,” alisema.

Send this to a friend