Tanzania kucheza na Colombia robo Fainali ya Kombe la Dunia

0
18

Timu ya Taifa ya Wanawake Chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls), inatarajia kucheza na Colombia katika robo fainali baada ya kuandika historia kwa mara ya kwanza kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuitoa Canada.

Mechi ya Robo Fainali baina ya Tanzania (Serengeti Girls) na Colombia inatarajiwa kuchezwa Oktoba 22, 2022 jijini Goa, India.

Akizungumza mara baada ya mchezo kumalizika, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul ameishukuru Serikali kuwezesha timu hiyo ya Serengeti kuanzia kuweka kambi ya kutosha katika Mji wa Southampton nchini Uingereza ambapo ilifanya maandalizi mazuri ambayo yameifikisha hapo timu hiyo.

Historia na mataji ya Club Africain aliyopangiwa kucheza na Yanga SC

“Nawapongeza sana wanangu hawa, wameliheshimisha Taifa, wameitangaza Tanzania, sasa hivi sio Royal Tour peke ake inayoweza kuitangaza nchi yetu bali hata Sekta ya michezo imeiweka Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye vipaji na kujulikana zaidi” amesema.

Kwa upande wa Kocha Bakari Shime, amesema wasichana wamefanya vizuri baada ya kufuata maelekezo aliyowapatia pamoja na kurekebisha makosa waliyoyaona katika mechi zao mbili za kwanza, huku akisema wasichana hao siku zote wana ari ya ushindi na wamekua na utulivu kiakili pamoja na nidhamu ya hali ya juu.