Tanzania kukumbwa na El Nino, hizi ni njia rahisi za kujikinga

0
31

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), El Nino ni mfumo wa hali ya hewa unaosababishwa na uwepo wa joto la bahari la juu ya wastani katika eneo la kati la kitropiki katika Bahari ya Pasifiki.

Hali hii kwa kawaida huambatana na vipindi vya mvua kubwa vinavyoweza kusababisha mafuriko.

Kila nchi kupitia mamlaka zake za hali ya hewa zimeanza kutoa taarifa ya tukio hili la asili linalotokea kila baada ya miaka kadhaa baada ya kuonekana kwenye mifumo yao ya hali ya hewa.

Nchini Tanzania Mamlaka ya hali ya hewa nayo imethibitisha kwamba inatarajiwa kukumbwa na El Nino.

Fahamu namna ya kujiadhari na athari mbaya zitokanazo na El Nino;

1. Hakikisha unapata habari kutoka huduma za hali ya hewa na taasisi za kitaifa za ufuatiliaji wa El Niño. Hii itakupa taarifa muhimu kuhusu hali ya El Niño na jinsi inavyoendelea.

2. Hakikisha unahama kwenye maeneo ya mabonde hasa nyakati za mvua zinapoanza.

3. Weka akiba ya maji. El Niño inaweza kusababisha ukame katika maeneo fulani na mvua kubwa katika maeneo mengine. Weka akiba ya maji safi na salama kwa matumizi ya nyumbani na kilimo, haswa katika maeneo yaliyo katika hatari kubwa ya ukame.

Utafiti mpya: Unywaji pombe wa wastanii hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo

4. Jenga miundombinu ya kupambana na mafuriko. El Niño inaweza kuleta mvua kubwa, ambayo inaweza kusababisha mafuriko. Jenga miundombinu inayofaa ya kupambana na mafuriko, kama vile mifereji ya maji, mabwawa ya kuhifadhi maji, na mifumo ya kusambaza maji.

5. Epuka kukaa, kutembea sehemu hatarishi kama kwenye mikondo ya maji na umeme hasa kipindi cha mvua na upepo mkali.

6. Ikiwa unaishi katika maeneo yanayoweza kuharibiwa na mafuriko au mmomonyoko wa ardhi, hakikisha unafanya ukaguzi wa nyumba yako na kufanya marekebisho yoyote muhimu. Unaweza pia kuhitaji kuhamisha mali yako ili kuepuka madhara.

7. Kuwa na mawasiliano ya watoa huduma za dharura, ya majirani zako na ya kiongozi wako wa eneo unaloishi.

8. El Niño inaweza kuathiri uzalishaji wa mazao. Kupanda mazao yanayostahimili hali ya hewa mbaya na kufuatilia tahadhari za kilimo kunaweza kusaidia kupunguza athari za El Niño kwenye kilimo.

Toa taarifa kwa Mamlaka inapotokea dharura yoyote katika eneo lako unaloishi.

Send this to a friend