Tanzania kupeleka wanajeshi kudhibiti waasi DR Congo

0
49

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amesema kwa kiasi kikubwa wananchi wamesaidia kuwafichua magaidi ambao walikuwa miongoni mwa jamii.

Mabeyo ameyasema hayo katika mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini na kusema kuna baadhi ya wananchi waliathirika, kuharibiwa mali na wengine kutekwa na vikundi vya ugaidi.

“Adui haonekani waziwazi lakini kwa kushirikiana na wenzetu na wananchi kwa ujumla, tumeweza kukabiliana na hali hiyo vizuri sana. Mpaka sasa tunataka kuhakikisha mpaka wetu uko salama” amesema.

Serikali yapitisha pendekezo la bima ya afya kwa watu wote

Mabeyo amesema kutokana na hali ya michafuko inayoendelea katika nchi ya Demokrasia ya  Congo, Jeshi la Tanzania limekubali kuwasaidia kuondoa michafuko inayoendelea.

“Kwa bahati mbaya majirani zetu wanakabiliwa sasa na tishio hilo kwa kiasi kikubwa, na sisi kama sehemu ya ukanda wa SADC tumekubaliana kwamba tutawasaidia wenzetu na sisi tuna vikundi vyetu kule bado tunaendelea kupambana” amesema.

Ameongeza kuwa mipaka ya Tanzania haijaathiriwa kutokana na migogoro inayoendelea pamoja na vitendo vya ugaidi  katika nchi za Rwanda na DR Congo.

Send this to a friend