Tanzania imeazimia kushirikiana na nchi jirani za ukanda wa Afrika ambazo bado zina viashiria vya virusi vya ugonjwa wa Polio ili kuutokomeza na kujihakikishia usalama dhidi ya ugonjwa huo.
Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Hassan Hafidh, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Tume ya 34 ya Kanda ya Afrika kwa ajili ya kutokomeza Polio (ARCC), Jijini Dar es Salaam ambapo amesema Tanzania ilianzisha Kamati za Kitaifa za Polio ili kufuatilia na kutoa usaidizi wa kitaalamu kuhakikisha nchi zinazoizunguka ziko kwenye njia ya kufikia malengo ya kutokomeza polio.
“Tanzania imepiga hatua kubwa katika kutokomeza polio, kesi ya mwisho iliyothibitishwa kimaabara ya WPV iliripotiwa mwaka 1996. Tuna mfumo wa ufuatiliaji ulioimarishwa nchini kote, unaoongezewa na maeneo 16 ya ufuatiliaji wa mazingira katika Mikoa 12, lakini Tanzania haitakuwa salama iwapo nchi jirani zinazoizunguka zitakuwa bado zina virusi vya polio,” amesema.
Ameongeza, “Kamati tatu zinazofanya kazi za polio zikiwemo, Kamati ya Kitaifa ya Udhibitishaji (NCC), Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu wa Polio (NPEC) na Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Polio (NTF) zilianzishwa. Kamati hizi huendesha mikutano kwa mujibu wa majukumu na hadidu za rejea (TOR), Kamati hizi za Kiufundi zimechangia pakubwa katika kudumisha mafanikio ya kutokomeza polio nchini.”
Madaktari bingwa wafanikiwa kuziba mfuko wa chakula wenye matundu mengi
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tanzania, Dkt. william Mwengee ambaye ni kiongozi wa timu ya chanjo na ufuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo, ametoa rai kwa wanajamii kuhakikisha wanashiriki uchanjaji ili kuhakikisha watoto wote wanakuwa na kinga ya pamoja.