Tanzania kusaini mkataba wa ushirikiano kufundisha Kiswahili Afrika Kusini

0
46

Tanzania na Afrika Kusini zinatarajiwa kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya elimu msingi katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7, ambapo kitaifa yatafanyika jijini Dar es Salaam.

Moja ya makubaliano yatakayowezesha kuimarisha ushirikaino kwa nchi hizo mbili ni pamoja na Tanzania kuisaidia Afrika Kusini kufundisha lugha ya Kiswahili.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini, Matsie Angelina Motshekga jijini Dar es salaam.

Haya hapa matokeo ya kidato cha sita na ualimu mwaka 2022

Waziri Mkenda amesema mkataba huo wa makubaliano unasainiwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya viongozi wakuu ambao ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa waliyoitoa ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu.

Ameongeza kuwa mara baada ya kusainiwa makubaliano hayo viongozi wakuu watakutana kwa ajili ya kuweka mpango kazi wa utekelezaji ili isiwe ni makubaliano pekee bali na utekelezaji wake pia.

Motshekga amesema, makubaliano hayo yatakuwa muhimu na yenye tija kwa Tanzania pamoja na wananchi wa Afrika Kusini ambao wanaipenda na kuithamini lugha ya Kiswahili.

Send this to a friend