Tanzania kusajili uwekezaji wa trilioni 37 kutoka nje ifikapo 2025

0
34

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imejiwekea lengo la kupokea uwekezaji wa dola za Kimarekani bilioni 15 [TZS trilioni 37.58] kutoka nje ya nchi (FDI) ifikapo mwaka 2025.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika Mkutano wa Biashara kati ya India na Tanzania huko New Delhi ikiwa ni ziara yake ya kitaifa ya siku nne.

Rais Samia ameeleza kuwa Tanzania imefanya marekebisho kwenye kanuni na sheria zake za biashara ili kuwa rahisi kwa wafanyabiashara wa ndani na nje kuzingatia pamoja na kufanya maboresho ya matumizi ya teknolojia ili kusaidia biashara mpya kusajiliwa kwa urahisi.

Pia, amesema Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania, imeanzisha dawati maalum kwa ajili ya kutoa msaada kwa watu na biashara kutoka nchini India.

Lengo la kupata uwekezaji wa dola bilioni 15 ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na India.

Wakati wa ziara hiyo, Tanzania na India zimesaini mkataba mmoja na hati za makubaliano 14 katika maeneo mbalimbali kama mawasiliano, usalama wa bahari na michezo na kadhalika, ambayo itaendeleza biashara kati ya nchi hizo mbili.

Ziara ya Rais nchini India inalenga kukuza ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili na kuleta manufaa kwa pande zote.

Send this to a friend