Tanzania kuuza gesi nje ya Afrika

0
49

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inatarajia kuuza gesi ndani ya Afrika na nje ya Afrika baada ya ujenzi wa mtambo mkubwa wa kuchakata gesi asilia (LNG) kujengwa mkoani Lindi.

Ameyasema hayo wakati wa mahojiano yake na Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando Ikulu Chamwino Dodoma, alipomuuliza kipi kinachoweza kuinufaisha Tanzania kati ya mishati ya gesi au nishati ya maji.

“Miaka mitano iliyopita tulifanya mazungumzo na wazalishaji wa LNG, ile gesi ya kutengeneza, kuchakata halafu iuzwe, hatukufanikiwa vizuri. Mwaka jana tukarudisha tena mazungumzo, nadhani mwezi wa sita mwaka huu tutasaini. Ule mtambo mkubwa wa kuchakata gesi hiyo utajengwa Tanzania kule Lindi,” amesema Rais Samia.

Aidha, amesema Serikali imefufua nishati ya gesi na tayari mazungumzo yana kwenda vizuri na wazalishaji.

Send this to a friend