Tanzania kuuza sukari nje ifikapo mwaka 2025

0
46

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeazimia kufanya mageuzi ya kilimo cha kisasa ambayo yanapaswa kwenda sambamba na mahitaji ya viwanda vya ndani ili kuifanya nchi iweze kuwa mzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo Afrika.

Ameyasema hayo leo alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Kagera kilichopo Misenyi mkoani humo.

Aidha, amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha alizeti na michikichi mkoani humo ili kuzalisha mafuta ya kujitosheleza ndani ya nchi na kuwawezesha vijana kujiajiri na kuinua uchumi wa Mkoa huo.

Hata hivyo, amewataka wawekezaji katika viwanda vya sukari nchini kuchangia kikamilifu kufanikisha malengo ya kujitosheleza na kufikia lengo la kuuza nchi za nje ifikapo 2025.

Rais Samia: Msiwabambike wananchi bili za maji

Mbali na hayo, amewataka wawekezaji kuiga mfano wa mwekezaji wa kiwanda cha Kagera Sugar kwa kuajiri vijana katika shughuli muhimu za kilimo ambao wengi wao ni wahitimu wa vyuo mbalimbali vya hapa nchini.

Send this to a friend