Tanzania mwenyeji mkutano wa Kimataifa wa Hamasa ya Nishati Safi Januari

0
17

Tanzania inatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Kimataifa kwa ajili ya uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi duniani, ajenda iliyochagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kinara katika uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi nchini na kote barani Afrika.

Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 31, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Hamasa ya matumizi ya nishati safi kwenye mkoani humo, ambapo ametoa wito kwa watanzania kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutumia nishati safi ya kupikia.

“Tumepata heshima ya kuuendesha mkutano wa kimataifa mwezi ujao wa kwanza hapa Tanzania, mataifa yote yatakuja Tanzania kwenye mkutano huo wa kampeni ya hamasa ya matumizi ya nishati safi,” amesema.

Waziri Mkuu amesema faida ya matumizi ya nishati safi ambayo ni gesi, umeme pamoja na makaa ya mawe, amesema Nishati safi inalinda afya ya Watanzania, kulinda mazingira dhidi ya ukataji wa miti pamoja na kutoa ulinzi kwenye nishati endelevu.