Tanzania na Malawi zasaini makubaliano ya ushirikiano katika mawasiliano

0
19

Tanzania na Malawi zimesaini hati za makubaliano (MoU) kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inayogusa masuala ya mawasiliano na digitali yakihusisha mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa intaneti kwa gharama nafuu kwa kuiunganisha Malawi na mkongo wa Taifa wa Tanzania.

Mkataba huo umeshuhudiwa na Rais Samia Suluhu pamoja na mwenyeji wake Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera baada ya mazungumzo yaliyofanyika baina ya nchi hizo katika Ikulu ya Kamuzu mjini Lilongwe nchini Malawi.

Rais Samia: Watanzania changamkieni fursa za ukuaji wa Kiswahili duniani

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye amesema Tanzania imedhamiria kutoa ushirikiano katika masuala ya usalama wa mtandao, upashanaji wa taarifa pamoja na kuunganisha nchi na watu wake.

Naye, Waziri wa Habari na Uhusiano wa Dijitali nchini Malawi, Moses Kunkuyu amesema kupitia uunganishaji huo, Tume ya Ugavi wa Umeme ya Malawi (ESCOM) na Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) zitapunguza gharama za uendeshaji, na hivyo kupunguza gharama ya jumla ya data kwa watumiaji.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ni sehemu ya ziara ya siku tatu ya Rais Samia nchini Malawi ambayo imehitimishwa leo.

Send this to a friend