Tanzania na Marekani zazungumza kuhusu kilimo

0
28

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Kate Somvongsiri katika Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo wamejadili kwa kina kuhusu vipaombele vya serikali katika wizara ya kilimo.

Pia, wamejadili umuhimu wa kutatua tija na uzalishaji mdogo kwenye mazao ya wakulima ili kutafuta mwarobaini wa kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini.

Kadhalika wamejadili umuhimu wa kuongeza nguvu na umuhimu katika sekta ya utafiti ili kubaini nini kinahitajika katika ardhi ya kilimo katika maeneo mbalimbali ya wakulima nchini ili wakulima waweze kutambua mazao yanayokubalika katika maeneo yao pamoja na kutambua aina na kiasi cha mbolea kinachohitajika.

Vilevile majadiliano hayo yamejikita zaidi kuhusu umuhimu wa kuboresha huduma za ugani, ambapo Waziri Mkenda ameeleza kuwa tayari wizara yake imeanza kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na kuwawezesha maafisa ugani kuwa na Pikipiki ambazo zitawarahisishia kuwafikia wakulima kwa wakati.

Aidha, katika mazungumzo hayo wamejadili umuhimu wa ugharamiaji wa kilimo (Agro Financing), pamoja na kuwekeza kwenye Kilimo Anga.

Bi. Somvongsi amemueleza mwenyeji wake kuwa USAID dhamira ya kushiriki katika kikao kazi hicho ni pamoja na kukutana nae ili kujitambulisha kwake kujua vipaombele vya wizara na kuandaa mkakati wa namna ya kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za Kilimo.

Send this to a friend